Mengi yamesemwa kuhusiana na mauaji ya Wagalla huku serikali ikidai kuwa idadi kamili ya watu waliouawa sio elfu tano bali ni 365. Hata hivyo maswali chungu nzima yanazidi kujiri kuhusiana na mauaji hayo. Je, ni kwa nini serikali iwageuke raia wake? na je, ni kweli kwamba wanajeshi wakenya walikuwa wakipambana na mashifta waliokuwa wakizua hali ya wasiwasi miongoni mwa wakenya?wengine wanadai kuwa jeshi la Kenya lilikuwa likilinda mipaka yake baada ya aliyekuwa Rais wa Somalia Siad Barre kuonyesha ishara ya kutaka kunyakua mkoa wa kaskazini mashariki. iwe ni mpaka au vita dhidi ya mashifta si haki kwa wanajeshi kuwabaka na kuwaua watu wake kiholela badala ya kuwafungulia mashtaka. Katika sehemu ya tatu ya makala haya mwanahabari wetu mpekuzi Mohammed Ali, anatafuta jawabu ya kutaka kujua iwapo baadhi ya watu mashuhuri waliozuru sehemu hiyo siku moja tu kabla ya mauaji hayo walikuwa wakijua ni yapi yangelijiri.